Na Zahara Tunda
Wadau mbalimbali wa usalama barabarani wakutana katika hatua
ya kupitia na kujadili mapendekezo ya kubadili baadhi ya vifungu vilivyopo kwenye
Sheria ya Usalama Barabarani ya mwaka 1973
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Bwalo
la polisi maeneo ya Oyster Bay.
|
Baadhi ya wadau wakifuatilia mapendekezo ya sheria ya usalama barabarani |
Mkutano huo uliongozwa na Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na
jeshi la polisi ilikusikiliza maoni ya wadau hao kabla ya kupeleke mapendekezo
rasmi kwa makatibu wakuu wa wizara na kuanza mchakato wa kuyafanyia kazi, ili
kupatikane sheria nzuri na yenye tija katika kuhakikisha kuna kuwa na usalama
barabarani.
|
Jones John akiwakilisha TCRF katika kuleta maoni kuhusu sheria usalama barabarani |
Asasi na taasisi mbalimbali kama mabalozi wa usalama
barabarani RSA TANZANIA, TAWLA, TABOA, TCRF, TLS, MOHA, TILDAF,
TCDRM, SHIVYAWATA, TMF pamoja na wawakilishi wa kutoka vyama vya madereva,abiria na wamiliki
wa daladala.
|
John Seka Mwenyekiti wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Tanzania RSA akitoa maoni |
Aidha na mwakilishi kutoka shirika la Afya Duniani (WHO) Bi
Mary Kessi alikuwepo katika kufanikisha na kusikiliza maoni na mapendekezo ya
wadau mbalimbali. WHO wamejikita katika kuhakikisha sheria mbalimbali za
usalama barabarani zinarekebishwa ili kuweza kupunguza ajali za barabarani
Tanzania na sehemu mbalimbali duniani.
|
Bi Joyce Momburi mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani akisikiliza kwa makini |
Mabadiliko ya sheria ya usalama barabarani yanatarajiwa
kupunguza ajali za barabarani, pamoja na kupunguza vihatarishi vinavyoweza
kumsababishia mtumiaji wa barabara madhara, yatakayo gharimu afya na uhai
wake.
No comments:
Post a Comment