Sunday, 8 October 2017

ELIMU YA VIZUIZI VYA WATOTO KATIKA MAGARI


                        
Na Zahara Tunda
Ni viti maalumu vilivyotengenezwa maalum kwa watoto kuanzia umri wa siku moja hadi miaka 12. Hivi viti vinawekwa katika gari ili kumkinga na kumlinda mtoto endapo ajali itatokea au gari litasimama ghafla.https://www.youtube.com/watch?v=uKwnh1jUHmU
            

Vizuizi hivi vimetengenezwa kwa kuangalia vigezo vya umri, uzito, umbo na urefu wa mtoto. Hivyo ni rahisi mzazi kupata kinachomfaa mtoto wake kutokana na umbo na umri wa mtoto wake.
Mtoto asipowekwa katika kizuizi cha mtoto anaweza kupata na mtikisiko wa ubongo,ulemavu nahata kupoteza maisha pindi ajali itakapotokea.

Wazazi wanajukumu la kumlinda mtoto katika magari yao ili kumwepusha na madhara yatokanayo na ajali za barabarani. Mzazi kwenye gari anajikinga kwa kufunga mkanda lakini mtoto hana cha kumlinda.


Wazazi wengi wanaimani kuwa wanaotumia vizuizi vya watoto ni wanaiga wazungu, ila ukweli ni kwamba hii teknolojia ya kuweka vizuizi vya watoto imechelewa kufika Tanzania. Na wachache tuu ndio wanamwamko wa kutumia vizuizi hivyo.
Lakini nia ya kuwepo kwa hivi vizuizi vya watoto ni kwamba iligundulika kuwa watoto wengi wanafariki na kupata matatizo ya akili au ulemavu pindi ajali inapotokea. Hapa ndipo vikatengenezwa na watu wenye magari wakashauriwa kuwa navyo ili kuwalinda watoto wao.



Nchi za kiafrika ambazo wana sheria inayowataka watumie vizuizi vya watoto ni pamoja na Ethiopia, Angola, Zambia, Msumbiji, Burkina Faso na Botswana. Licha ya Tanzaia kutokuwa na sheria hii ni jukumu la wazazi kuwalinda watoto wao na kuhakikisha usalama wao wakiwa kwenye magari.

Shirika la Afya Duniani WHO wanashauri wazazi kutumia vizuizi vya watoto ili kupunguza madhara ya mtoto kupata madhara makubwa pindi ajali itakapotokea.Mtoto anayewekwa katika kizuizi cha mtoto kwa usahihi anaweza kupunguza madhara ya ajali kwa asilimia 70 kwa watoto wachanga na 54% hadi 80 kwa watoto wadogo.

Ni wakati wa mzazi au mlezi unayemiliki gari kumlinde mtoto wake kwa kutumia vizuizi vya watoto. Wahenga wanasema “Kinga ni bora, kuliko tiba”. 

No comments:

Post a Comment

USALAMA WA WATOTO BARABARANI UTAZAMWE TENA

Kila mzazi au mlezi mwenye mtoto ni jukumu lake kuhakikisha usalama wa mtoto wake hasa aendapo shuleni na kurudi. Hii ni kutokana na maen...