Tamasha la sita la watu wenye ulemavu limefanyika Dar es salaam huku likikutanisha viongozi wa watu wenye ulemavu kutoka mikoa yote Tanzania.Ikiwa mwaka huu kauli mbiu ni kuhusu Tanzania ya viwanda, iweze kuzingatia upatikanaji wa fursa na mahitaji kwa watu wenye ulemavu.
|
Wadau mbalimbali wakifuatilia mada |
Tamasha hili limeandaliwa na Shirikisho la vyama vya walemavu Tanzania SHIVYAWATA kwa kushirikiana na taasisi ya The Foundation For Civil Society kwa kuwaleta pamoja watu wenye ulemavu kujadili na kupendekeza mapendekezo mbalimbali yanayowahusu watu wenye ulemavu ili kuendana na Tanzania ya viwanda.
|
Viongozi wa SHIVYAWATA pamoja na wadau wengine
|
Mwakilishi kutoka SIDO Halima Kazindogo alikuwepo kuelezea fursa zilizopo katika kuanzisha viwanda vidogovidogo kwa wajasiliriamali wadogo na akatoa wito kwa watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa zilizopo.
|
Halima Kazindogo mwakilishi kutoka SIDO akielezea fursa zilizopo
|
No comments:
Post a Comment