Monday, 26 March 2018

USALAMA WA WATOTO BARABARANI UTAZAMWE TENA


Kila mzazi au mlezi mwenye mtoto ni jukumu lake kuhakikisha usalama wa mtoto wake hasa aendapo shuleni na kurudi. Hii ni kutokana na maeneo mengi hasa ya karibu na barabara kuwa si salama kwa wanafunzi au watoto kutokana na kutokuwa na uhimizaji mkubwa wa masuala ya alama za barabarani na kuwepo kwa alama za barabarani.

Wazazi wajiepushe na kuwapandisha watoto wao chini ya miaka tisa katika usafiri wa bodaboda na wale ambao wanausafiri wao binafsi watumie vizuizi vya watoto katika kuhakikisha usalama wao katika vyombo vya moto.

Wanafunzi wakionyesha jinsi ya kuvuka Barabara

Katika uzinduzi wa barabara ya kupita wanafunzi pamoja na alama za barabarani zilizowekwa katika barabara ya shule ya msingi Mikumi iliyopo maeneo ya Magomeni mikumi. Ujenzi uliofadhiliwa na shirika la PUMA energy Tanzania, FIA Foundation na Amend. 
Jenista Mhagama, Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana, Ajira na walemavu ametoa wito kwa wadau wa usalama barabrani kuwakumbuka pia watoto walemavu katika elimu ya usalama barabarani kwasababu wote wanatumia barabara katika matembezi yao ya kila siku kuelekea shuleni.
Waziri Jenista Mhagama akizindua rasmi barabara ya kupita wanafunzi katika shule ya msingi Mikumi

Kuna kila sababu ya wazazi, walezi na wadau pamoja na serikali kuweke msisitizo katika kuchangia kutengeneza miundombinu bora kwa wanafunzi wanaotumia barabara ili waweze kuhakikisha watoto wao wapo salama muda wote wanapoenda shuleni.


Wanafunzi wenye ulemavu wakiimba wimbo wa usalama barabarani pamoja na waziri

Vilevile elimu ya usalama barabarani itolewe kwa wingi kwa wanafunzi madarasani ili waweze kuwa na ufahamu kuhusu alama za usalama barabarani wakiwa wadogo na hii kupelekea kupata mabalozi wazuri wa usalama barabarani.



No comments:

Post a Comment

USALAMA WA WATOTO BARABARANI UTAZAMWE TENA

Kila mzazi au mlezi mwenye mtoto ni jukumu lake kuhakikisha usalama wa mtoto wake hasa aendapo shuleni na kurudi. Hii ni kutokana na maen...