Monday, 26 March 2018

USALAMA WA WATOTO BARABARANI UTAZAMWE TENA


Kila mzazi au mlezi mwenye mtoto ni jukumu lake kuhakikisha usalama wa mtoto wake hasa aendapo shuleni na kurudi. Hii ni kutokana na maeneo mengi hasa ya karibu na barabara kuwa si salama kwa wanafunzi au watoto kutokana na kutokuwa na uhimizaji mkubwa wa masuala ya alama za barabarani na kuwepo kwa alama za barabarani.

Wazazi wajiepushe na kuwapandisha watoto wao chini ya miaka tisa katika usafiri wa bodaboda na wale ambao wanausafiri wao binafsi watumie vizuizi vya watoto katika kuhakikisha usalama wao katika vyombo vya moto.

Wanafunzi wakionyesha jinsi ya kuvuka Barabara

Katika uzinduzi wa barabara ya kupita wanafunzi pamoja na alama za barabarani zilizowekwa katika barabara ya shule ya msingi Mikumi iliyopo maeneo ya Magomeni mikumi. Ujenzi uliofadhiliwa na shirika la PUMA energy Tanzania, FIA Foundation na Amend. 
Jenista Mhagama, Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana, Ajira na walemavu ametoa wito kwa wadau wa usalama barabrani kuwakumbuka pia watoto walemavu katika elimu ya usalama barabarani kwasababu wote wanatumia barabara katika matembezi yao ya kila siku kuelekea shuleni.
Waziri Jenista Mhagama akizindua rasmi barabara ya kupita wanafunzi katika shule ya msingi Mikumi

Kuna kila sababu ya wazazi, walezi na wadau pamoja na serikali kuweke msisitizo katika kuchangia kutengeneza miundombinu bora kwa wanafunzi wanaotumia barabara ili waweze kuhakikisha watoto wao wapo salama muda wote wanapoenda shuleni.


Wanafunzi wenye ulemavu wakiimba wimbo wa usalama barabarani pamoja na waziri

Vilevile elimu ya usalama barabarani itolewe kwa wingi kwa wanafunzi madarasani ili waweze kuwa na ufahamu kuhusu alama za usalama barabarani wakiwa wadogo na hii kupelekea kupata mabalozi wazuri wa usalama barabarani.



Saturday, 11 November 2017

Elias Mutani aibuka kidedea katika mashindano ya Burt Award

Burt award ni mashindano ya hadithi kwa lugha ya kingereza yanayolenga hadithi zitakazosomwa na watoto au wanafunzi kuanzia miaka 12 mpaka 18, rasmi yalianzishwa mwaka 2008 kwa Tanzania, mashindano haya yana ratibiwa na Children Books Project (CBP).
Mwaka huu mshindi ni Elias Mutani ambaye kitabu chake cha The little Missionary with Golden paper knife kimeibuka kidedea.


Elias Mutani akipokea zawadi na mkono wa pongezi kutoka kwa mgeni rasmi.

Mgeni rasmi Habib Sentu kutoka Taasisi ya Elimu akitoa salamu zake kwa wageni waliohudhuria halfa ya ugawaji tuzo.
Kushoto Mwenyekiti wa Bodi ya CBP Abdulahi Saiwaad, Pili Dumea katibu mtendaji CBP, mwandishi nguli Richard Mabala, Elias Mutani, Habib Sentu, Gabriel Kitua kutoka PATA na mwandishi Nahida Esmail.






Richard Mabala akiweka sahihi katika kitabu kama ishara ya uwepo wake na kuweka ushawishi kwa wanafunzi kupenda kusoma vitabu vya hadithi.


Mshindi Elias Mutani katika picha ya pamoja na wanafunzi na mwalimu wao kutoka Tambaza Sekondari.

Saturday, 4 November 2017

"Tanzania ya Viwanda" Izingatie Upatikanaji wa Fursa kwa Watu Wenye Ulemavu

Tamasha la sita la watu wenye ulemavu limefanyika  Dar es salaam huku likikutanisha viongozi wa watu wenye ulemavu kutoka mikoa yote Tanzania.Ikiwa mwaka huu kauli mbiu ni kuhusu Tanzania ya viwanda, iweze kuzingatia upatikanaji wa fursa na mahitaji kwa watu wenye ulemavu.

Wadau mbalimbali wakifuatilia mada 







Tamasha hili limeandaliwa na Shirikisho la vyama vya walemavu Tanzania SHIVYAWATA kwa kushirikiana na taasisi ya The Foundation For Civil Society  kwa kuwaleta pamoja watu wenye ulemavu kujadili na kupendekeza mapendekezo mbalimbali yanayowahusu watu wenye ulemavu ili kuendana na Tanzania ya viwanda.

Viongozi wa SHIVYAWATA pamoja na wadau wengine
Mwakilishi kutoka SIDO  Halima Kazindogo alikuwepo kuelezea fursa zilizopo katika kuanzisha viwanda vidogovidogo kwa wajasiliriamali wadogo na akatoa wito kwa watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa zilizopo.
Halima Kazindogo mwakilishi kutoka SIDO akielezea fursa zilizopo

Friday, 20 October 2017

BODI YA KISWAHILI KUSINI MWA AFRIKA YAZINDULIWA RASMI AFRIKA KUSINI


Na Zahara Tunda
Bodi ya Kiswahili Kusini mwa Afrika imezinduliwa siku ya Heritage day nchini Afrika ya Kusini mjini Cape Town, lengo la bodi hiyo ni kukuza na kutangaza Kiswahili kusini mwa Afrika na afrika kwa ujumla.
Vilevile lengo lingine ni kutengeneza misingi sahihi ya kukiingiza Kiswahili kama lugha ya Afrika katika ngazi ya shule ya msingi mpaka sekondari na chuo kikuu.Kutumia lugha kama chombo cha kudumisha umoja na ushirikiano kati ya nchi na nchi.Kuboresha masuala ya kiuchumi, kisiasa na kijamii
Kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa lugha ya Kiswahili Afrika.

Waziri Mstaafu wa Mazingira na maji Afrika Kusini Bi Buyelwa Sonjica akiongea na wajumbe



Baadhi ya wajumbe wa bodi ya Kiswahili Kusini mwa Afrika 

Dr.Zukile Jama, mwenyekiti wa bodi ya Kiswahili Kusini mwa Afrika ambaye pia ni mwalimu katika chuo kikuu cha Cape Town katika masuala ya African languages.

Tuesday, 17 October 2017

SUMATRA YATOA TUZO KWA WASAFIRISHAJI BORA WA ABIRIA

Na Zahara Tunda

SUMATRA yatoa Tuzo kwa watoa huduma wakubwa  na wakati wa mabasi ya mkoani. Makampuni yaliyopata tuzo hizo ni pamoja na Shabiby Line, Kilimanjaro Express, BMcoach, Kimbinyiko,JM Luxury na Satco Express. Tuzo hizo ni baada ya kushindanisha watoa huduma ya usafiri kwa masafa marefu.
Mwakilishi wa Shabiby Line Akipokea Tuzo Kutoka kwa Makamu wa Rais


Mwakilishi wa Kilimanjaro Express Akipokea Mkono wa Pongezi
Mwakilishi wa Kampuni ya BM Coach akipokea Cheti kwa niaba ya Kampuni yao
Mwakilishi wa Kampuni ya  Kimbinyiko Akipokea Tuzo ya  Watoa Huduma Wakati











WIKI YA USALAMA BARABARANI: Ajali Sasa Basi

Wiki ya usalama barabarani imefunguliwa rasmi na makamu wa Rais Samia Suluhu na maadhimisho hayo yanafanyika mkoani Kilimanjaro katika viwanja vya mashujaa.
Makamu wa Rais akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa polisi na waziri wa Mambo ya Ndani

Wadau kutoka sehemu mbalimbali wameungana katika kutoa elimu na huduma mbalimbali kuhusu usalama barabarani.
Irene Musellem kutoka RSA Tanzania akiwapa elimu ya usalama barabarani katika banda la Mabalozi wa Usalama Tanzania

Gerald Erasto kutoka Anglogold ashanti  (GGM) akitoa elimu ya usalama barabarani katika banda lao la maonyesho 
Mhandisi Leonard Saukwa kutoka Wizara ya Ujenzi akitoa elimu kuhusu barabara kwa watoto waliokuwa katika maonyesho
Maadhimisho hayo yalipambwa kwa maandamano ya madereva mbalimbali
Madereva Bodaboda katika maandamano
Mabalozi wa Usalama Barabarani wakiwa katika maandamano katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa Usalama Barabarani

Friday, 13 October 2017

WADAU WA USALAMA BARABARANI WAKUTANA KUJADILI MAPENDEKEZO YA MABADILIKO YA SHERIA YA USALAMA BARABARANI SURA YA 168

Na Zahara Tunda

Wadau mbalimbali wa usalama barabarani wakutana katika hatua ya kupitia na kujadili mapendekezo ya kubadili baadhi ya vifungu vilivyopo kwenye Sheria ya Usalama Barabarani ya  mwaka 1973 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Bwalo la polisi maeneo ya Oyster Bay.
Baadhi ya wadau wakifuatilia mapendekezo ya sheria ya usalama barabarani


Mkutano huo uliongozwa na Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na jeshi la polisi ilikusikiliza maoni ya wadau hao kabla ya kupeleke mapendekezo rasmi kwa makatibu wakuu wa wizara na kuanza mchakato wa kuyafanyia kazi, ili kupatikane sheria nzuri na yenye tija katika kuhakikisha kuna kuwa na usalama barabarani.
Jones John  akiwakilisha TCRF katika kuleta maoni kuhusu sheria usalama barabarani

 Asasi na  taasisi mbalimbali kama mabalozi wa usalama barabarani RSA TANZANIA, TAWLA, TABOA, TCRF, TLS, MOHA, TILDAF, TCDRM, SHIVYAWATA, TMF pamoja na wawakilishi wa kutoka vyama vya madereva,abiria na wamiliki wa daladala.
John Seka Mwenyekiti wa Mabalozi wa Usalama Barabarani Tanzania RSA akitoa maoni 

Aidha na mwakilishi kutoka shirika la Afya Duniani (WHO) Bi Mary Kessi alikuwepo katika kufanikisha na kusikiliza maoni na mapendekezo ya wadau mbalimbali. WHO wamejikita katika kuhakikisha sheria mbalimbali za usalama barabarani zinarekebishwa ili kuweza kupunguza ajali za barabarani Tanzania na sehemu mbalimbali duniani.
Bi Joyce Momburi mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani akisikiliza kwa makini


Mabadiliko ya sheria ya usalama barabarani yanatarajiwa kupunguza ajali za barabarani, pamoja na kupunguza vihatarishi vinavyoweza kumsababishia mtumiaji wa barabara madhara, yatakayo gharimu afya na uhai wake.

USALAMA WA WATOTO BARABARANI UTAZAMWE TENA

Kila mzazi au mlezi mwenye mtoto ni jukumu lake kuhakikisha usalama wa mtoto wake hasa aendapo shuleni na kurudi. Hii ni kutokana na maen...