Kila mzazi au mlezi mwenye mtoto ni jukumu lake
kuhakikisha usalama wa mtoto wake hasa aendapo shuleni na kurudi. Hii ni
kutokana na maeneo mengi hasa ya karibu na barabara kuwa si salama kwa
wanafunzi au watoto kutokana na kutokuwa na uhimizaji mkubwa wa masuala ya
alama za barabarani na kuwepo kwa alama za barabarani.
Wazazi wajiepushe na kuwapandisha watoto wao chini ya miaka tisa katika usafiri wa bodaboda na wale ambao wanausafiri wao binafsi watumie vizuizi vya watoto katika kuhakikisha usalama wao katika vyombo vya moto.
Wanafunzi wakionyesha jinsi ya kuvuka Barabara |
Katika uzinduzi wa barabara ya kupita wanafunzi pamoja na
alama za barabarani zilizowekwa katika barabara ya shule ya msingi Mikumi iliyopo
maeneo ya Magomeni mikumi. Ujenzi uliofadhiliwa na shirika la PUMA energy
Tanzania, FIA Foundation na Amend.
Jenista Mhagama, Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana, Ajira na walemavu ametoa wito kwa wadau wa usalama barabrani kuwakumbuka pia watoto walemavu katika elimu ya usalama barabarani kwasababu wote wanatumia barabara katika matembezi yao ya kila siku kuelekea shuleni.
Waziri Jenista Mhagama akizindua rasmi barabara ya kupita wanafunzi katika shule ya msingi Mikumi |
Kuna kila sababu ya wazazi, walezi na wadau pamoja na serikali kuweke msisitizo
katika kuchangia kutengeneza miundombinu bora kwa wanafunzi wanaotumia barabara ili waweze kuhakikisha
watoto wao wapo salama muda wote wanapoenda shuleni.
Wanafunzi wenye ulemavu wakiimba wimbo wa usalama barabarani pamoja na waziri |
Vilevile elimu ya usalama barabarani itolewe kwa wingi kwa
wanafunzi madarasani ili waweze kuwa na ufahamu kuhusu alama za usalama
barabarani wakiwa wadogo na hii kupelekea kupata mabalozi wazuri wa usalama
barabarani.